Community Values
Community values held by the Bajunity community

The community values are passed from one generation to the next. Culturally, while the father took responsibility of teaching community core values to the boys, girls were taught by their mother or grandmother. Any parent in the community could also teach values because children are the responsibility of the community. The other space for teaching of values is through religious teaching in the madrasa. Disputes were resolved through elders or religious leaders.
This section develops these ideas further.
Maadili
Maadili hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na ni jukumu la mzazi /wazazi kuwafunza watoto wao maadili. Mtoto wa kiume alikuwa akifundishwa maadili na mzazi wake wa kiume ilihali mtoto wa kike alikuwa akifundishwa maadili na mzazi wake wa kike au hata nyanyake.
Kwa Wabajuni vilevile, mzazi yoyote yuwaweza kumkanya mtoto wa mwenzake, yaani kila mwanajamii ana jukumu la kumwelekeza mwana wa mwenzake. Mbinu hii ya ushirikiano ilihakikisha kwamba watu wazima wote katika jamii walitoa mwongozo na uelewa thabiti kwa watoto. Tofauti na wakati wa sasa ambapo kufunza maadili na kuadhibu watoto wanaofanya makosa unafanywa na wazazi waliowazaa.
Vilevile watoto huwa hufunzwa maadili chuoni ambapo huwa wanaenda kusoma Quran na pia watoto hao baada ya kutoka chuoni huenda madrasa ambapo husomeshwa masomo mbalimbali yanayofundisha watoto hao maadili.
Watoto hufundishwa kazi mbalimbali wanaopokuwa chuoni kama vile:Kutapasa majamvi, Kuenda kuni, Kusuka usitu, Kuteka maji n.k
Kusuluhisha Migogoro
Majirani wanapokosana, migogoro ilikuwa ikisuluhishwa na waliokaribu kwa kuwapatanisha waliogombana. Iwapo vita ni vikubwa mno na haviingiliki, wazee ndio huhusishwa. Wazee huja na kuwapa mawaidha waliokosana na kusuluhishwa migogoro hiyo na watu hao hupatanishwa.
Wazee wanapokuja kusuluhisha vita hivyo, huwa hawataki kujua sababu ya migogoro hiyo kwani watakaporudisha mambo hayo ya nyuma basi migogoro hio haingepata suluhu. Hivyo basi wazee hao huwapatanisha na fatiha hutiwa na hupeanana mikono na kusameheana. Iwapo wazee wameshindwa kabisa kusuluhisha vita hivyo basi walimu wa dini walihusishwa kwenye kusuluhisha.