Economic Activities Pt. 1
The economic activities and related cultural practices of the Bajuni community. This article focuses on farming.

As part of their cultural heritage, the Bajuni undertake farming and fishing activities. Young people are socialized into these activities. Farming among the Bajuni is associated with the ritual performances of Vave and Randa both of which are performed in preparation for cultivation.
While the Vave was performed before the clearing of the bushes, the Randa was performed after the successful undertaking of the communal task. This section discusses the ritual preparation of farms, boat making, fishing, weaving, mangrove cutting, carving and other socio-economic activities of the Bajuni.
Ukulima
Unapofika wakati wa kulima, kwanza kabisa hutoka mwana-chuoni akiandamana na watu kadhaa kuenda kutembea mwituni kuangalia ni sehemu gani ambayo watalima na kuchagua sehemu ifaayo kulimwa.
Baada ya kuchagua sehemu hiyo, Wabajuni hibika kuo, yaani kuweka mistari ya kugawanya kila mmoja sehemu yake ya kulima. Baada ya muda wakulima hao hutengeza boma karibu na mashamba yao ya kuishi pamoja kwa kipindi kile cha kulima.
Wakati wa kuchema/kukata msitu, Wabajuni hualikana na yule mwenye kukata msitu huo anapokuwa shambani hupelekewa mkate wa kijojo na majirani zake mpaka anapomaliza kukata msitu huo.
Baada ya kumaliza, kukata msitu, sasa watu hualikwa na kuambiwa kuwa ni wakati wa kupisa/ kuchoma msitu. Watu huja pamoja na usiku wa kuamkia siku ya kupisa/kuchoma msitu, kuna sherehe ambapo ngoma ya vave huchezwa usiku wote na asubuhi yake msitu huchomwa.
Baada ya kuchoma msitu, Wabajuni hucheza ngoma ya randa ambayo hupigwa kwenye kila mlango wa mkulima na wale wenye nyumba hutoa zawadi kuwapa wapigaji ngoma.
Mfano wa Randa:
Rigombo rigombo rigombo,
Chacha rigombo
Kwerekeche wana ware
Chacha rigombo
Wakati wa kuvuna, yale mahindi ya kwanza ambayo huitwa cheche hugawanywa kwa majirani kwanza kabla ya mwenye shamba kupeleka mahindi nyumbani kwake na mengine kupelekwa msikitini.
Vifaa vya Ukulima
- Kitoka: ni chuma ambacho hutiwa makali na kutengezewa/kutiwa kwenye mpini na
hutumika katika kukata miti. - Sali/ mashoka madogo
- Majembe
Miko ya Kibajuni inayohusiana na ukulima
Baada ya wakulima kulima mashamba hayo yalikuwa yakifungwa. Wakati wa kufunguliwa mashamba hayo /konde hizo atakwenda mwanamme barobaro akojolee kisiki. Sababu ya kukojolea kisiki ni kuwa sasa hivi mtu yeyote anaweza kuingia kwenye shamba hilo, yaani limeshafunguliwa.