Mafumbo ya Kibajuni

Kibiriti cha ndaṯi, huenda yuu chikiaiṯi, chikipua chunda mbiṯi, ni cha ndrove
nakwambia.
Kibiriti cha ndathi humaanisha mchi
Huenda yuu chikiaiṯi humaanisha Wakati wa kuponda, ule mchi huenda juu
na chini.
Chikipua chunḏa mbiṯi yamaanisha kuwa baada ya kupondwa ule wishwa
hutoka na mahindi hubakia na kuanikwa.

Kisima cha binpai na noka wa kivuwai, nae hasidi wa mai na hicho nacho
chambua.
Kisima cha binpai humaanisha taa ya kandili.
Noka wa kivuwai humaanisha utambi uliopo kwenye kandili
Mai humaanisha mafuta ya taa yaliyopo kwenye kandili