Mashairi a Kibajuni
Mashairi 139 yanayozungumzia masuala ya kijamii ya Kibajuni

Mashairi a Kibajuni ni kitabu cha kipekee na cha mara ya kwanza
kuchapishwa kwa lahaja ya Kibajuni (Kitikuu) moja kwa moja. Pia
tahajia iliyotumika ni ya Kibajuni na haijasanifishwa kwa sababu
juhudi za usanifishaji wa lahaja bado hazijakamilika, ijapokuwa
zimeanza.
Ndani humu mna mashairi mia moja thelathini na tisa (139)
yanayozungumzia masuala mbalimali ya kijamii – historia, maadili,
mahusiano, kazi, mazingira na kadhalika. Kama itakavyodhihirika,
washairi wengi wamebobea katika tungo za tathlitha (mishororo mitatu
kwa ubeti).
Wabajuni wananasibishwa na tungo kama vile vave, randa, kimai,
na gungu. Baadhi ya mashairi yao ni ya kujibizana. Kutokana na
mabadiliko ya kijamii tungo za kimapokeo zinapotea licha ya juhudi
ya kuzihifadhi. Juhudi za kuimarisha tungo za Kibajuni na kuhuisha
tungo za kale ni muhimu sana. Kitabu hiki ni sehemu ya juhudi hizo.
Sifa ya Kibajuni ni kuwa Wabajuni wanajifahiri na lahaja yao. Hili
linajitokeza humu