Mashairi ya Jumla
Mwana natoka hondreni, jiko halikwishwa kwenga,
Hondre icheledhe jani, utekeze na mapema
Na hii ni ramadhani, nasi chwataka kufunga
Shauri gani malenga, talimwaye hondre hii
Ukitaka na langu lima, na ramadhani ufunge
Uandike ingo ine, na utekeze mapema
Ufanye na jitihadi, usimamie vachumwa
Na papa kulijainya, uwawanya wakulima
Ukitaka langu lima, na ramadhani ufunge
Nalikuva kivunda kuni, hata mocho siyavasa
Hata kidhunguka ṉima, hava vachu hunegesa
Lau kama mpumbavu, chambo ingalinasa
Iva nani baumudhi, tevu hulia makosa
Ni kama umbula Bereki, kiapo nichiliecho
Tabika mwichu kidari, na Simambae siketi
Haendi magendo Pemba, ela nipawe cheti
Salamu dha Muhammadi, na Mdasiru wa Shali
Mbwa wafanya walimu, kusomesha na kuswali
Nja huva hayaumbwa, kadara hwandikwa mbali
Mwanangu mbwa bei wakununuliwa,
Lakini mambo ni majaaliwa,
Nchendri huchendra hangoji kwambiwa.
Alhamdulilahi, namshukuru jalia,
Matakwa niyatakavyo, ndriye ndo nitimidhia,
Saa indonifuacha, nendrapo tasikilia.
Hunena Halima Sidhi, hadhineni hunenewa.
Ukashika na ubachi, kusudi kulikemea.
Vidhi vashishie chaa, havaisi kujepea.
Nataka sipachi, la kunisha hamu,
Nishike kibachi, sawa na mwalimu,
Nikalie kachi, niise karamu.
Maskini maskini, Mwanasha wa Buvae
Na shauri mi sina, mwenye kula nae
Fumo sina na Njahidi sinae.
Maskini mwanasha wa nkunguru,
Hana kimo wala hana kinyunguru,
Upindrene kama nsindhi wa vuru.
Maskini mwanasha wa maboriṯi,
Nkokoni nalikwendra kwa kaniki,
Fumo sina, Njahidi simuisi.
Ukingia, hungia kwa utiriri
Ukasimama nlangoni, hukwambia biri
Na kesi dhake ni ngumi, hadhichiliki wakili
Bahari ina ngurumo na madhoruba na pepo,
Kuna na sera maini, iṯo nalienge hapo,
Siaṯe dhela na dhama, ikiva akili iko
Sambuku huenda ndrama, ingiapo nkondroni,
Na papa huanika ṯenevi, na videge makokoni,
Ndooni nchege jarifa, ya udhi wa lailoni
Wawapi wapaṯe shungwa, waungwana wa hiari
Wako ndrani ya miṯanga, liwafungile kaburi,
Kaa ukizingatia, dunia ina ghururi
Fatima wa mwalimu, nipa muṯo nipindruke,
Na sigara na sigara, unisumbie nivuche
Inwa chai inwa chai, kiṯoka unikumbuke
Pembe binti halifa, imi nalikuchendani,
Sigara na kibiriti, kampilichi medhani
Kafanye mashughuli vako, kisha unienge nami
Iṉi mulioko darakasi, maneno medhoyasikia,
Numba hadhifuki mosi, wala hadhivaki taa,
Chendwee nferejini, chulumbisie kutwaa
Iṉi mulioko darakase, maneno mudhoyasikia,
Kwa kula mweṉe akili, anyuke andame nḏia,
Isi hulisonga dona, vake vechu huumia
Hakuna kadhi habithi, kama kadhi a uṯonyi,
Usiku chuko maini, na nṯana chuko imboni,
Nafurahike Hadhija, Tima uko nlangoni
Habari yenu Chovae, Kiunga nisikidhie,
Suala na thamanini, Pwani salama dhiie,
Nikuvee sikwanguka, lakini niumdhie.
Ningidhie mapueni, na mashadha kuniṯinda,
Dhema ndilo kosa langu, ajali haina kinga
Chendra wema nende dhako, usingoje shukurani.
Nimepiga lindi, shubiri na nyanḏa nne,
Kaiṯaraji na vua, haramu isinye,
Fadhila ni mbeu mbovu, vakulima msilime.
Undrugu wa siku hidhi, hauṯaki muafaka,
Una dhitwa za jauri, na ruhuma za kupaka,
Hakikachiki kinofu, imi changu ngalikikacha.
Mwenye pupa hadiriki kula tamu,
Japo wampa, hula na zamzamu,
Mzoea mihogo, wali haumuelei ṯamu
Kenda washishie chama, vatonyi husikitika,
Licha kupacha kupima, hata kibobwe cha kuoka,
Lichombosee iema, na angiae huṯoka
Singombanii kisiki, kisichoota majani,
Wewe kwangu si iliki, wala mdalasini,
Ukijiona pilau, wenzio biryani
Hengeva mekacha kamba, simba mepaa angani,
Sacho medonwa na yondra, kiboko mengia Pwani,
Papa mechagadha namba, ndriye simba nsichuni
Umasikini uovu, heri usiku wa kidha
Hukwondolea kidhadhi, ukakosa na kabila
Mungu ndie atoae, siwedhi kunvulidha
Bule ndhivie nyawe, ushari wake sitaki,
Na Disii (DC) ni mpiya, takwendra kunshitaki
Humusi Muhamadi, Rukiya tampachapi
Alhamdullilah ndrivyo ilivo ilivo dunia
Nalikivaa dhikandu, dhiachu na sidiria,
Eo kifua kaniki, usipache ya kuanikia