Mashairi ya Kunyoza (Sega/ Baṯi)
Poetry to prepare the bridegroom for the marriage ceremony.

Yomi mame yomi mame, Mwanasha wa Bavuae
Na shauri na shauri, sina mwenye kula nae
Fumo sina fumo sina, na n'jahidi sinae.
Nalimfanya ni nchu, kanchia maanani
Karama ni mvundifu, menivundia jirani
Kuku usinpe wisha, hashibi ela yaani.
Haa hunipacha imi, mweṉe haya na ruhuma
Kaya kasimama nao, siwedhi kuasukuma
Shirika halina wema, na nla pweke hakuna.
Kuna nnyama baharini, ina lake huchwa kasa
Una dhijaa dhinne, cha tanu huocha sasa
Pale ṯini a kikovu, kuna kichu nakitaka.
Mambo a vanasiasa, amenichia udhia
Vafanyao nda makosa, na vakali kivambia
Ntudhi ni wa kudasa, huchundrae kunyavia?
Vaume na vanavake, nipani nami yakini
Nambiani nitosheke, maana ake a ndrani
Yondra kutovona lake, husababishwa na nini?
Taibikae kidari, na kupasua kifua
Nikudhidi utiriri, mwishoe kuichomowa
Dharuba ngava si nduri, nalo shuari huvua.
Dhioja dhake bahari, nahodha medhielewa
Chomboche mekisairi, na changale melichuwa
Pepo dhingava hatari, hata shuari huvuwa.
Hidhi dhisa na mikasa, ni ada ulimwenguni
Na kupacha na kukosa, ndrio ake mitihani
Siisumbue kunosa, haanweki mai pwani
Kukwambia imebidi, ukweli uuchambuwe
Na wala si makusudi, ni tabia ako uwe
Na hasidi changu jadi, hufa iye ama ndruwe.
Kuvinḏa ni kuikisi, shabaha kuipachia
Kauchambuwa wepesi, medhani kaichumia
Hulia nadho rasasi, mwanapaa mekimbia.
Mambo ataka wakati, mbioni usiichie
Tena kuna na bahaṯi, hilo usilililie
Livivie si iviti, ila usinichilie.
Taikadha tusicheche,sitaki la kukufuru
Nitayaata yapiche, liyalo nitashukuru
Ni ajabu kwa kiveche, kwa kun'teka kiguru.
Simwandami ibilisi, na vaja kajibidhana
Ni muungwana halisi, sina chembe a uchwana
Ishashopoka rasasi, hairudi nyuma tena.
Ni udhicho kula tena, na siwedhi kuienga
Kwa sasa ladha haina, roho angu ishazinga
Haluwa si tamu tena, imeingia n'tanga.
Chengedha dhako kauli, usimamapo kunena
Uichudhe na akili, unene yenye maana
Usiifanye dalali, na vanunudhi hakuna.
Nchu huonya dhichendo, na mambo kwa ufanisi
Tuheshimu vadhalendro, venye asili halisi
Havavi sawa kwa mwendro, mwanapunda na farasi.
Hana kiwango cha namba, Kwa udhuri umefika
Nina haki kujigamba, Kwa anavo nawirika
Si nnene si mwembamba, Huu wangu malaika.
Umasikini muovu, heri usiku wa kidha
Hukwandolea kidhadhi, ukakosa na kabila
Mola hatoi kwa safu, siwedhi kunvulidha.
Sivue mato sienge, ukaanguka ndiani
Heshima ako itunge, sihadawe mwafulani
Uliambiwa kitenge, ukakichia nchoni.
Valianda kwa dhishindro, sungura na kina paka
Na ndivo vachu va mwando, valoanda kuniteka
Kweli kobe hana mwendro, na atakapo hufika.
Imi nahodha halisi, kila bandari najua
Huivucha mikambisi, na papa venye hatua
Iweje uwe kiṯasi, wataka kunisumbua.
Ukiugua fuadi, kapache akupendae,
Ukisikia baridi, eka mocho kwenye gae,
Nambieni huu hasidi, nimpe ni kimfae?
Uzuri wa mwananke, ni vuso na nchilinga,
Katika kifua chake, mavili makoma manga,
Unacho kitana chake, hutania n'ee singa.
Mwenechu mwanahalima, sinitafudhie voe,
N'chu yambo huamdama, akaiva ukomoe,
Baba nakilima chake, asokilima ni shoe.
Kuna ikoko la wimbi, na nchama na mafucha,
Mai hubika idhimbi, na mikondo akuvucha,
Kama mepacha n’ngine, nami Mungu atanipa.
Sinione kunyamaa, ninganena na kuteka,
Moyo hauna furaha, na wala sikuudhika,
Kunichonesa jaraha, afadhali kunibika.
Afadhali kunibika, kavona husuka damu,
Na dawa nikiandika, akufaa kafahamu,
Na hilo litoe shaka, sifi kwa ulimi tamu
Sinione kunyamaa, si n'chache wa fahamu,
Hukuata kusikia, mambo yalojiri Amu,
Avavie kisimani, na n'tungini sitamu.
Kama siisi kusoma, mwalimu sinidharau,
Ubongo wangu kitwani, hauhitaji nahau,
Saumu angu ninao, nilie kwa kusahau.
Mame aliponidhaa, hakunipeka chuvoni,
Alinipa sufuria, nikaingia mekoni,
Jeneresheni akisasa, mapenzi kitotoroni.
Habari ako nipeche, idhidie kunivua,
Na mambo anikemeche, sikuwedha kuchachua,
Nataraji uwe peche, kwa baraka na afua.
Tukua salamu fundi, mwenye kanisalimie
Mueledhe kwa udhuri, maneno ayasikie
Yana nandikiwa chai, kiinwa inidhurie.
Kiva ni mpija mbao, korija mbili nataka
Niundrie kijahadhi, chakuendrea Mambasa
Asili ikanidhuru, ina mafucha a kasa.
Hoko boni la bonita, vaboni vana uchesi
Vengi vamehasirika, na vengine ni uyusi
Nimuene yondra huteka, tavau hunyua nyusi.
Rabi sinipe mapenzi, vapendwao hakuna
Valobaki majambazi, vapicha vakijivuna
Vamebaki menyo wadhi, kipichacho huchafuna.
Nimezie kufahamu, sitokutiriri tena
Lakini nakulaumu, kuchenda yaso maana
Utakuja lishwa sumu, kwa kupenda bure sana
Mapenzi humea wapi, nendre ḵayapalilie
Niyafulie makopwa, na mai niyachilie
Ivapo wema hulipwa, kwanda ningelipwa mie.
Sitaki kidhee, aenendao kwa gongo
Nataka kijana, awedhae mambo
Ukimpa chombo, takivusha ng’ambo