Mashairi ya mapenzi

Hata shilingi alifu, nambia imi nilipe
Mwili wako dhaifu, sitaki utaabike
Hata ndrani mwa kaburi, nivilia nakuchike
Mwichu nalishika gongo, kaipigia na ina
Na mai ali hakuna, kafukua na kisima
Hondre dhikiva na nḏovu, huṯukidha vakulima
Mbegu ya huba ni maṯo, lindi ni moyo kupenda
Mfanye na jitihadi, ya kusafisha dhivanda
Vua ni ulimi wako, yembe ni nkono kwendra
Nalimpenda Buraki, kwa daraja na murua,
Kamfanyia safari, ya ndrege si ya mashua,
Ni nḏicho chumbi a mawe, nimechoka kutukua.
Mweṉewe sikuridhika, ina kuichwa Buraki,
Melikata tangamano, imi nawe tena basi,
Kama upeche faidi, kama ukosedha basi.
Nendra kufunga idundu, sitaki tena machembe,
Nisimame nlangoni, apichao anienge,
Nyuka utoke ndhee, sinifanyie tenge.
Nke hupendwa tabia, hatamaniwi machembe,
Utafanya bina gani, hata vachu vakuenge,
Ninyukapo kwendra dhangu, siagi sifanyi ṯenge
Pepo zikivuma, naliko kidhisikia,
Zikikoma, hufanya shaki kalia,
Mbona huba usiku hunizidia.
Bini nalikuchambua, pale ukifanya shaki,
Huba usiku hudhidi, hupungua nṯikachi,
Lakini huumia, mweye kupenda kwa dhati
Hukesa na yondi yeo, fenusi ni la nchambo
Nipache na mahashiki, wanipumbaze kwa nyimbo
Salamu mpe mpendi, na rubani mwene chombo
Mwenechu Bwanamkuu, mpendi uniposee
Vachu vote hunena, na haya uikosee
Nenda kwamwambia mame, shagadhio yandee
Saa sita za ntana, kipacha kui hulia
Kula kitaka kushuka, luki hunidhivia
Iṯo langu ndilo lako, niengea malikia
Mame Javo, nipemba name mwanao
Unipembe moyo, uwe na pumbao
Kama fume hakuanguka, tanbika apichao
Fuma mai, Shanga nende kwa maguu
Nimpembe, asilie mwana huu
Nadho ndrani na inḏe, zimenivunḏa maguu
Ndrege tukua salamu, mpe Tima Madhei
Ntakuya imi pweke, wala nchu sidhengei
Mwana ukiteka Chula, hufurahi Ashuwei
Rohashani na Zubeda, kuna vana va maina
Kwanḏaa Makai Umari na Malinganya na Dina
Muovu ndrimi Marua, wakunipa mai sina
Abasi wa Dilimua, nipe kishiko nishike
Mbeu ikiharibika, tia samani nilipe
Mahaba hununuliwa aso shilingi adhikwe
Nina vanangu vachachu, nivafanyie nkache
Kwanḏa ni wavee radhi, nivatufie na mache,
Rehema na Mwahila, fundi wavo Mwanase
Mvundeni kuna zijana merini
Kuna vatinḏaji nee na watinḏaji sakini
Nkipeche dilimuo chakula takula imi
Hema dhenyu dha kidhungu, mweṉewe nichambudhie
Ifudhi wa pembe ine, kachikachi inyusie
Heri nambie sitaki, sikitiko sinichie