Mashairi ya Vugo

Unani rafiki yangu, mbona undokwonda hiya
Metokwa na michilinga, kwa fikira dha dunia
Mwanamume ni ntudhi, kila ncho huchovea
Wahaiba wahaiba, nyuka chwandame upepo,
Matilaba matilaba, ni hapo chuvonanapo
Ukishiba ukishiba, ndripo akili iyapo
Sitoshona sitoshona, sanda mahaba kadhika
Kavechea wenzangu, wasije wakaniteka
Sina nyonda sina nyonda, na kiva nalo taveka
Dhaungama Dhaungama, kidhipicha hudhirai
Garseni siendi, ndia dhishishie mayi
Nipa bure nikusifu, nikopesha unidai
Mame nipokea mwana, nendre dhangu machangani
Ninkimbie nvuli, mwene utukivu nami
Huniṯunda nipikacho, na nichiacho kanwani
Nalikwendra kutawadhi, kwa mayi yasioshaka
Na nsikichi karibu, kautapia haraka
Mangaribi sikuswali na Isha sikuipacha.
Yomi mame yomi mame, nipeche mahaba sumu
Hanipendi hanipendi, hanitunukii tunu
Pendo langu pendo langu, ahera takulaumu
Mwenechu bwana wa sumu, Nyuka chwendwe dhechu Amu,
Chukavaenge vadhungu, vapikavo dhichu tamu,
Ukichia shaka nno, halali huva haramu
Taniboi Taniboi sema neno nisikie, Nikujibu nikujibu au niinyamalie
Nikuwene si dereva, gari lako nichwadhie
Jabalini jabalini, nalifukua kisima
Makusudi makusudi, nipache mayi a kunwa
Ni haini ni haini, Binadamu si wema
Nendra kwa mwalimu wangu, alonisomesha sana
Akanichia igomba, naliko kikutamana
Nichelee sikuanguka, nipeche pa kusimama
Muhamadi muhamadi, Nakupenda sina shaka
Kanijengea na ṉumba, mfano wa madirasa
Nkache hula kidiku, na nusu humpa paka
Muhamadi muhamadi, Ina la sayidinaa
Tanlea niwedhavo, hata kwa wisha na kaa
Ukinvona nbike, na yama ngodhi hufaa
Unenee uni modi, Tchunda niwene namina
Namuua niiweneo, kidhingichini hamua.
Nimuene ikurabu, weadrao kuswali juma
Mame kinambia chua, nalimwambia sivoni
Kamwambia waayiva mahaba ni chundramboni
Mwana akipenḏwa nno, hudhia ama haponi
Nalikwendra koa pwani ufuoni,
Kadhama kadhuka na vanda matoni
Hudhengela lulu rangi ya paoni
Usiku wa yana nalihangaika
Kaandika chai ndrani ya birika
Nalidhani mbwangu kumbe mbwa shirika
Ndridhi kisukari, tamu kwa dhabibu
Nalipokutaka nalikujaribu
Sasa sikutaki toka taratibu
Sufi sio pamba, hebu pambanua
Na paka si simba, dhidi kuelewa
Wafitaje mimba na mwana hudhawa
Bosi langu si bosi la masihara
Hachafuni wala havuchi sigara
Raibika nami ningie hasara
Yailahi mueche mpendi wangu
Na mahaba adhidi kwake na kwangu
Siku dhote chuvaudhi valimwengu
Bwana hunambia usiku mbwa mwedhi
Tamu ya sukari si tamu angidhi
Nguvo a hariri si nguvo a udhi
Nendrapo harusini nguvo angu ṯaṯaua
Sivai a kuraruka vaja vakaniumbua
Sasa nimepacha simu sitaki tena barua
Bwana una ila chachu, Ndrudhangu hamunyisi
La kwanza ni mbaranganya
La pili hana dhabiti na
La chachu nivambie una ijungeni
Hapo dhamani dha kale, Vadhee vakiivana
Vakipika huliana, vakiwaa huadhana
Chundoharibu dunia, chuiyepo isi vana
Muhamadi Muhamadi, tantahiri kwa ng’ombe
Majirani majirani, vote ntudhi vaonde
Noni vote vakidona, kisumbikidho ni shongwe
Husikia minong’ong’ono, nimechia bina gani
Mushikene na mikono, muketi dhibaradhani
Muswalivo swala tano, na ahera mba mochoni
Munenavo muna nguvu Binadamu vapudhi
Muhadadhiwa kwa mache, na ulimi na pumudhi
Anipindriao maṯo ṯanpicha sinvudhi
Ukipacha mitihani, ndrivo kuiva dunia
Huiva akupendao, na aliyekutukia
Hata ukachendra wema, kwavo huva ni hatia
Vaso haya vaso haya, nyuso dhavo dhijeree
Ni lipi yambo la bina, ambalo niliesee?
Mukiwedha avanyani, langu fungu munechee
Ndruo muwenge uhai, umvulidhe habari
Umwandike na nkono, unyive ake hali
Singoje siku a kufa, mukachia yunguwadhi
Lahaula x2 moyo hauna kifiniko
Kitupani x2 wino umetawanyika
Hunambii x2 kama hujui kwanḏika?
Fahimu fanya heshima
Sinchukane Nggunya
Ngunya ni sulutwani
Kama umeshiba dona
kafue mayi ngamani