Methali na semi za Kibajuni (1)
Proverbs and sayings of the Bajuni community.
- Usivone dhombo kupicha na ungama ulimui.
- Wako kimpa mai wa ndruo muenge sana.
- Rafiki hukusaidia kwa kula hufawa na ndhawa nawe ikupachapo ghafula.
- Damu si mai.
- Usibike dhumbe ungama huyaiva ulipo.
- Ajali haina kinga
- Chendra wema wendre dhako
- Mwenye pupa hadiriki kula ṯamu
- Alimao mmoya walai ni vangi
- Ukivunḏa ada utadhaa kwa shida.
- Ṯamu iko kachika uṯungu.
- Rivu haipachi nke.
- Jirani ni aula.
- Shaba kushindra dhahabu elewa ni kidunia
- Kuna nadhi nnadhini wala makumbi haina
- Akufukudhae hakwambii ṯoka
- Akufaae kwa dhiki ndrie rafiki
- Kilio hulia mweṉe na nchu mbali kalia
- Shirika halina wema na nla pweke hakuna
- Kama halifuliwi mayi na mataruma hudhama