Methali na semi za Kibajuni (2)
Proverbs and sayings from the Bajuni community.
- Inyueni changa chwendeni, baharini si nkao
- Ukuru ni yaa
- Kuvunḏika kwa koleo sio mwisho wa uhunḏi
- Avavie kisimani na nṯungini si tamu
- Kila mwamba ngoma ngodhi huvuchia kwake
- Nianisie kuuma dhidhidie kuva mai
- Nlio wa ṉoni ausikiao ni ṉoni.
- Ukicha mwana kulia mwisho utalia uwe
- Alie mekoni ndrie adhimae mocho
- Mwendra ṯedhi na omo marejeo ni ngamani
- Ambacha ukucha punda weyao
- Nṯedha kwavo huchudhwa
- Mupembavo vana venyu na vangu nipembeani
- Kikuu hukua kwavo pembe humea kiṯwani
- Adhidhieo haisi hunena usuluhie
- Sacho uko ishimoni ikinda humidha vachu
- Nchu havi nchu mpaka ave na kichu cha kumpa nchu
- Nchu nkwavo
- Akupeo kichi uwe ndrie anipeo ikumbi
- Nchu ndrue