Methali na Semi za Kibajuni (3)
Proverbs and sayings from the Bajuni community.
- Upecheo ndriwe
- Ṉumba ikosao nshindo mwana hanyamai
- Usiku nmwangala ntumbuu huva papa
- Ṯaṯedhae na Mwarabu na iguu lenyu imoya.
- Kuketi si kama kwendra
- Nvundaṯi ni mwanaṯi
- Akukachae nsipa nawe nvunde mfupa
- Sinbike shoe dhicha ndrie mboni wa dhia
- Nchu ni ndrue na damu haifuchiki
- Samaki mpija mashudhi hakangwi kwa mafucha ya ucho
- Ni mocho hakubisiki dhidi mbuyu uye Pwani
- Ndhinga dhinga hukucha na mwendati hukuvaa
- Dhifudhao ni dha Rwabi, endhi dha nja hukoma
- Mai a pwani huvava na atavava daima
- Iganda la muwa la yana ṯungu mefanya ni pacho
- Mgagaa na upwa hali wali nkavu
- Usiaṯe mbachao kwa nswala upichao
- Ishe kunvaka inya valivadhaa vana
- Nchi nviṯi sipandre na nkavu sirevereve
- Avavie kisimani na nṯungini si ṯamu