Methali na Semi za Kibajuni (4)
Proverbs and sayings of the Bajuni community.
- Ulie wali bario uchekechee nkono
- Aso kuveko na lake haliko
- Umasikini si ila nchu ndrue hanṯeki
- Mungasumbuka vaja alie mbee u mbee
- Nchu nkukuche mwengeni maṯo
- Ukipawa kula ila kwa kuiva na ipawa lina miva
- Alivachao mai hali nchupu
- Nchu ndrue hanyavi ni akiba a kesho
- Ukenda nyi wa ṯongo lako iṯo funga.
- Ṯungu angamea mbava makadhi ake ni iṯi
- Twahara ya ijumaa hufanywa hamisi
- Nchu nkwavo japo ṯini mwa irara.
- Vachu vote vanganyuka isi huiyaliani?
- Nchu ndruwe haṯa kama udhidhie
- Ichumbo liloshiba halichambui alodhaa
- Ukimvona kobe menyamisa kiṯwa uive hupanga sheria
- Bahari ikichafuka madhimbi henda nsako
- Gonga igogo ulisikie nlio
- Dha kale hadhinuki
- Nla nawe hafi nawe ile ndhaliwa nawe