Methali na Semi za Kibajuni (5)

Proverbs and sayings from the Bajuni community.

  1. Sichie dhema nṯanga siku adhiki hufaa
  2. Aṯangae na yuva huyua
  3. Usiaṯe kadhi kabla a kupacha kadhi
  4. Vanishishie ombe natamani koa
  5. Kunewe kunyua pipa utasie kuchomoka
  6. Kipai cha jaha ni cha nja kuvakwa
  7. Iṯeke la kuku halimuumidhi mwanawe
  8. Nkunḏe isi angali nviṯi
  9. Kwene vadhee hapaharibiki yambo
  10. Mwenye nalo hangoji kuambiwa
  11. Ni yako ilio na doa roho angu nṉeupe
  12. Nchu duniani hucheswa na chake
  13. Mui huva mwema
  14. Kama nkweli nṯimidhie onyesha uvuli wako