Nyimbo za Kibajuni za Kumpemba Mwana
Here are some lullabies from the Bajuni community.

Kwa Wabajuni, nyimbo za kupemba mwana huweza kueleza hisia za yule mama anayempemba mwana, yaani hueleza yale yaliyo moyoni mwake.
Mfano wa nyimbo hizo ni:
Howa howaa nakuongoa,
nyamadha mwana kulia.
Kua mwana Mariamu, nikupeke madirasa,
Wende kapache elimu, usome na kuswalisha,
Utii vadhadhi vako , upache mema maisha.
Takupeka madirasa, nikupeke na sukuli,
Ukisha masomo ako, upache shahada mbili,
Huku ukiva imamu, na huku uve wakili.
Kwanda nalilipa deni, kimalidha kakopesha.
Na mimi ni maskini, sina bengi la mapesa,
Juya lishishie taka, samaki inde huteka.
Nimesikia kusi na dhishindro,
Kavulidha huko inde kunani,
Kaambiwa ni mumeo melalia kondro,
Mekuovolea nke mwanamwali,
Na mahari ake ntundo
Nalikwenda kutembea, sehemu za mbachu mbachu
Nikavona ng’ombe hutindwa, mwili hufanywa dhiachu,
Mwananke wa magendro, mahaba ni siku chachu.
Penda tu idha nifahamu,
Sinipende kwa idhilali si tamu,
Hakiliki chenye shaka ni haramu.
Dharura zikinibika, sikukosea fahamu,
Nilikaribu na pwani, hunengelea kastamu
Vuka jahazi wenendre, dhama nishe hamu.
Ukiya kwa wema, takupa nchumwa,
Akwandame nima, wendrapo chuvoni
Ukiya kwa pacho, takupa upecho
Wamenyo machocho, uchie shingoni
Silie usiku ndia dhina vachu,
Dhina vaswalina na vachavo Mungu
Mwanangu wa pacho, lia upendapo,
Takupa upecho, wa menyo machocho
Utie shingoni.
Hasidi ni ndruo muhasidiwae
Hapenḏi memayo, wala nukusani
Hapenḏi upache, wala upakache
Na mocho ufuke, kwako kijumbani
Silie usiku, ndia dhina vachu
Dhina waswalina na wachovu mungu
Hao waswalina wakali mbee, na wachavo mungu wakali nyuma
Na wachavo mungu tamko lavo, Inna Allaha maaswabirina
Wangu muja iwa na saburi, Inshallah takujali mema
Takujali ijara ya yusufu, aloishi ndani ya kisima
Aloishi kwa kudura Allahu, zamzamu mai ya kunwa
Mame mwana wangu, niombea mungu
Nivuke na changu, bandari salama
Nivuke na nyasi, na micho michesi
Kwenye mato asi na …….
Mame mwana wangu, niombea Mungu
Kiva na uṯungu, nidhae salama
Nidhae simba, kivumi cha ṉumba
Au kipinga ndrege wa shani
Mwanangu Suo silie, kilio cha daima
Menitoka nchilinda, nami nchilinda sina
Simuudhi Mwanaidi, Mwana bibiye mbwa inya.