Shivulani ni Shaulani

Shivulani ni Shaulani

Shairi la Shivulani ni Shaulani linatupeleka katika safari yenye
kina na maki. Mohamed M. Kombo anatumia sanaa ya hali ya
juu kurejelea masuala muhimu kwa jamii ya Wabajuni huku
akitumia mtindo wa uneni ili kuwasilisha ujumbe wake. Mbinu
hii ya uneni ni ya kimazungumzo na inamwezesha msanii huyu
kuwasiliana moja kwa moja na hadhira yake. Ameifinyanga
lugha ya Kibajuni kwa usanifu mkubwa na kutumia jazanda,
mafumbo, taswira na tamathali ili kuteka hisia za msikilizaji
na msomaji wa tungo zake. Bila shaka msomaji wa Shivulani ni
Shaulani atafurahia uhondo uliomo humu.