Traditional medicine

The Bajuni had their traditional medicine for all sorts of ailments. The medicine is part of the traditional knowledge that is getting lost. This section mentions some of the medicine.

Dawa za Kiasili na Matibabu

Matibabu ya piso

Piso ni chuma ambacho hutengezwa kwa umbo fulani na kutiwa motoni mpaka kinapokuwa chekundu na kisha kinapokuwa moto, mtu huwekwa kwenye ile sehemu iliyo na ugonjwa.

Matibabu ya kuumikwa kwa pembe.
Matibabu ya kuchanjwa
Matibabu ya wali wa ito

Huu ni aina ya wali ambao hupikwa kwa mchuzi wa samaki / ng’onda maalum (Tewa, Mbawaa, Tanumbaa na Nkoma) na huliwa alfajiri. Wali huu hutibu ugonjwa wa hasadi/jicho ovu.


Baada ya kula, huwa kuna vinu vya maji ya kuosha mkono na kusukutuwa kisha ukishamaliza kusukutuwa yale maji kwa mdomo hutemwa kwenye kinu kingine. Yule mwenye ugonjwa huo wa jito baya huwekwa kitini na kufinikiwa nguo na kumwagiwa maji yale yaliyotemwa baada ya kusukutua.

Matibabu ya homa

Miti ya matibabu ya homa mbalimbali ni pamoja na : kaumwa, mjafari, liwa, koto na mnuka uvundo.
Miti hii hutumiwa kutibu homa mbalimbali kama vile homa ya matumbo, kichwa n.k.

Mfano:
Dawa ya mfukufuku ambayo majani yake yaliwekwa kwenye jiwe la moto na kusagwa mtu akafungwa nayo tumboni.
Kaumwa ilitumika kuponya mshipa ikiwa ulikuwa ukiumwa.
Mti wa mvumbani uliponya presha, kisunzi, bokhari.
Salamaki ilitumika ikiwa mtu alikuwa na maumivu ya tumbo.